test

NAIBU WAZIRI REGINA NDEGE ATIMIZA AHADI YA MILIONI 1 KWA VIJANA WA BAJAJI BABATI



Naibu Waziri wa Utumishi na Utawala Bora na Mbunge wa Viti Maalum Mkoa wa Manyara, Mhe. Regina Ndege tarehe 19 Juni 2026,amekabidhi kiasi cha Tsh. 1,000,000/= kwa vijana wa Bajaji Babati Mjini.


Fedha hizo ni utekelezaji wa ahadi aliyoitoa wakati wa Mbio za Mwenge wa Uhuru 2026 Babati Mjini, kufuatia pendekezo la Kiongozi wa Mbio za Mwenge Kitaifa, Ndg. Wazo.

Akizungumza wakati wa makabidhiano, Mhe. Regina amesema lengo la mkopo huo ni kuwawezesha vijana hao kujikwamua kiuchumi. Aidha amewataka kikundi hicho *kufungua Gereji* ili waweze kujiongezea kipato pamoja na kutoa ajira kwa vijana wengine.










Hata hivyo *Mhe Jitu* alipata wasaa wa kuelezea vijana wa Bajaji fursa ya ufundi gereji kupitia *VETA* na kuwahidi kuwaunganisha na fursa kubwa ya ujuzi wa ufundi bajaji

Makabidhiano hayo yameshuhudiwa na *Mwenyekiti wa UWT Mkoa, Ndg. Fatuma Tsea*, Diwani wa Kata husika, Viongozi wa Vijana na Viongozi wa Serikali za Mitaa.
NAIBU WAZIRI REGINA NDEGE ATIMIZA AHADI YA MILIONI 1 KWA VIJANA WA BAJAJI BABATI NAIBU WAZIRI REGINA NDEGE ATIMIZA AHADI YA MILIONI 1 KWA VIJANA WA BAJAJI BABATI Reviewed by VISION MEDIATZBLOG on July 19, 2026 Rating: 5

No comments:

Powered by Blogger.