test

SILLO AKABIDHI PHOTOCOPY MASHINE ENDAKISO

 

Mbunge wa Jimbo la Babati Vijijini na Naibu Spika wa Bunge, Daniel Baran Sillo, ametimiza ahadi yake kwa kukabidhi mashine ya photocopy katika Shule ya Sekondari Endakiso, Kata ya Endakiso, ikiwa ni hatua ya kusaidia kuboresha mazingira ya utoaji wa elimu shuleni hapo.




Mashine zilizokuwa zikitumika shuleni hapo zilikuwa hazikidhi mahitaji kutokana na idadi kubwa ya wanafunzi, hali iliyokuwa ikisababisha changamoto katika upatikanaji wa nakala mbalimbali, ikiwemo mitihani na nyaraka nyingine za shule.


Akizungumza wakati wa makabidhiano hayo,Mkuu wa Shule ya Sekondari Endakiso, Nadhili Ally Sadallah, amemshukuru Naibu Spika Sillo kwa kutimiza ahadi hiyo, akisema mashine hiyo itarahisisha shughuli mbalimbali za shule na kuwezesha kupata nakala za kutosha za mitihani kwa ajili ya wanafunzi.


Kwa upande wake, Diwani wa Kata ya Endakiso, Hassan Dodo  amesema kata hiyo inaendelea na juhudi za kuboresha miundombinu ya elimu, ambapo kwa sasa kuna ujenzi wa madarasa manne unaofadhiliwa kwa mchango wa wananchi.


Amesema pia kuna ujenzi wa hosteli ya wasichana katika Shule ya Sekondari Endakiso kwa msaada wa wadau STC, huku akimshukuru Naibu Spika Sillo kwa kuendelea kushirikiana na wananchi na kusaidia kutatua changamoto zinazowakabili katika sekta ya elimu.


Aidha, Naibu Spika Daniel Sillo ameahidi kukabidhi tanki lenye ujazo wa lita 10,000 kwa ajili ya kuhifadhia maji katika Shule ya Sekondari Endakiso, hatua inayolenga kuongeza upatikanaji wa maji na kuboresha mazingira ya shule.

SILLO AKABIDHI PHOTOCOPY MASHINE ENDAKISO SILLO AKABIDHI PHOTOCOPY MASHINE  ENDAKISO Reviewed by VISION MEDIATZBLOG on August 12, 2026 Rating: 5

No comments:

Powered by Blogger.