Naibu Spika wa Bunge na Mbunge wa Jimbo la Babati vijijini Mhe. Daniel sillo amewaomba viongozi wa Dini wazidi kumuombea ili aweze kutekeleza majukumu yake Kwa ufanisi.
Mhe Sillo ameyasema hayo Leo katika Hafla MAALUMU ya pongezi iliyo andaliwa na vijana katika Kata ya Galapo, kwa ajili ya kumpongeza kiongozi huyo.
Aidha sillo ameahidi kuendelea kushirikiana na viongozi wa Dini wa kimila pamoja na makundi mbali mbali pasipo kuwabagua.
Hafla hiyo iliambatana na Maombi kutoka Kwa viongozi hao huku wakiahidi kuendelea kumuunga mkono Mhe. Sillo na kumuombea ili aweze kufanikisha adhma ya maendeleo katika jimbo la Babati Vijijini na Taifa Kwa ujumla
Vile vile SILLO ameahidi kufanyia kazi Changamoto za vijana alizozipokea kupitia Risala ya vijana hao.
" VIONGOZI WA DINI MZIDI KUNIOMBEA" MHE SILLO.
Reviewed by VISION MEDIATZBLOG
on
August 10, 2026
Rating:
Reviewed by VISION MEDIATZBLOG
on
August 10, 2026
Rating:






No comments: