test

CHAMA CHA BISIGYE CHA KATAA MARIDHIANO NA SERIKALI YA MUSEVENI.

 Chama cha Peoples Front for Freedom (PFF) kinachoongozwa na wafuasi wa mwanasiasa wa upinzani nchini Uganda, Dk. Kizza Besigye, kimesema hakiko tayari kushiriki mazungumzo ya kisiasa yanayolenga kutafuta suluhu ya kesi zinazomkabili mwanasiasa huyo.



PFF imesema kwa sasa haina mpango wa kukaa mezani kwa mazungumzo hayo, ikieleza kuwa baadhi ya viongozi wake wanakabiliwa na matatizo ya kiafya. Chama hicho pia kimehoji uwezekano wa kufanya mazungumzo na watu ambacho kinawashutumu kwa kuhusika na vitendo vya kuwadhulumu viongozi wake.


Msimamo huo umetolewa wakati zikitimia miaka miwili tangu Dk. Besigye na Obed Lutale wakamatwe jijini Nairobi, Kenya, kisha kupelekwa Uganda. PFF inaeleza kuwa tukio hilo lilikuwa ni utekaji nyara.


Naibu Katibu Mkuu wa chama hicho, Kennedy Okello, amesema hali ya kiafya ya baadhi ya watu wanaoshikiliwa ni miongoni mwa sababu zinazofanya chama hicho kisione mazingira ya kuanza mazungumzo kwa wakati huu.


Dk. Kizza Besigye bado anashikiliwa nchini Uganda akikabiliwa na tuhuma za uhaini.



CHAMA CHA BISIGYE CHA KATAA MARIDHIANO NA SERIKALI YA MUSEVENI. CHAMA CHA BISIGYE CHA KATAA MARIDHIANO NA SERIKALI YA MUSEVENI. Reviewed by VISION MEDIATZBLOG on November 17, 2026 Rating: 5

No comments:

Powered by Blogger.